From the recordings BHALO LIVE IN TANZANIA and ALL JUMA BHALO'S SONGS
Lyrics
SINA NENO SINA NENO
ELA AMRI YA MNGU
MOYO WANGU WANIN’GA KAMA MWEZI
LA MATUNGU SINA TENA SIKU HIZI X2
PENDO LANGU LIMEPATA MTUKUZI
SINA NENO SINA NENO ELA AMRI YA MNGU
MTUKUZI MWEMA ALO NA IMANI
MSIKIZI MKUMBUKAJI HISANI X2
MPUMBAZI WA TABIYA NA LISANI
SINA NENO SINA NENO ELA AMRI YA MNGU
LA AJIZI KWAKE HALIPATIKANI
NI MJUZI MSARIFU NA MAKINI X2
MLIWAZI HAPANA CHEKE KIFANI
SINA NENO SINA NENO ELA AMRI YA MNGU
ILO WAZI SITOWATA KUBAINBI
MPUMBAZI ALIYE MWANGU MOYONI X2
SIKU HIZI SINA NENO ASILANI
SINA NENO SINA NENO
SINA NENO SINA NENO
ELA AMRI YA MNGU