HARUFU YA NUNIEWE HARUFU YA NUNI MPENZI FANYA IMANI


NAKUPA ILO HAKIKA           - EWE HARUFU YA NUNI
KWAKO NIMESWALITIKA - HALIYANGU TAABANI
NISEZE KUFEDHEKEKA - KWA HUBA ZAKO FULANI


USIKU KUCHA SILALI - HUWA MATO KITANDANI
NA MTANA KUTWA SILI - CHAKULA SIKITAMANI
PENDO LANIPA THAKILI - NIWAHI NITAABANI


FANYA HIMA UNOKOWE -UNITOWE MATESONI
SINA DAWA NYENGINEWE - HILI NAKUPA YAKINI
LAU SIKUPATI WEWE - SITOPOWA ASILANI

SIKUDHANIA ASILI KUWA TANIGEUKIYA

SIKUDHANIA ASILI KUWA TANIGEUKIYA
LAKINI UNGANIDHILI ITAFAKURI DUNIYA


1 KUHIMILI MAUDHIKO  ***YASIO KUWA NA NDIYA
NA MAOVU MATAMKO  ****YA MATUNGU KUNITIYA
MOYO WANGU MBLE YAKO**** KABISA SIKUDHANIA


2 TANGAMANO NILOKIRI  ***** KUISHI NAWE PAMOYA
KIDHANI LITANAWIRI ********LIZIDI KUENDELEYA
KUMBE LAJA NIKHASIR*****I KISIMANI KUNITIYA


3 MAWAZO NILIYOWAZA ***** NIKAWA NA SAFI NIYA
NA MANGI KATEKELEZA ****** BILA NYUMA KUREGEYA
KUMBE KWAKO NAWA PWEZA ******MOTO NAJIPALILIYA4 UDHULI NA SONONEKO****** MOYONI ULONITIYA X2
UNGANETESA MWENZAKO****** SIKITU TAVUMILIYA
LEO KWANGU KESHO KWAKO***** INA MALIPO DUNIYA5 MATESO UNITESAYO****** PASI KUNIHURUMIYA
NA PENDO LAWANGU MOYO***** AMBALO WALIONEYA
SIKUDHANI KUWA HAYO *******UTAKUJA NITENDEYA


 KUSHUKURU MOLA WANGU***** NAOMBA KUENDELEYA
NA KUHILMILI MATUNGU************ MOYONI NIGAUMIYA
LILO NDIKWA NA MNGU************ SIWEZI KULIZUWIYA7 TAMATI NAKHATIMISHA *******ZAIDI SITOKWAMBIYA
NAWEWE UNGANITWESHA *******MAZITO HAYA NA HAYA
HAKUNA LISILOKWISHA************ ITAFAKURI DUNIYA

SIKUDHANIA ASILI
SIKUDHANIA ASILI KUWA TANIGEUKIYA
KANAMA WEWE HUJALI MAPENZI KUYAONEYA
LAKINI UNGANIDHILI ITAFAKURI DUNIYA

NAJA NIKO SAFARINI

NAJA NIKO SAFARINI – NAWE NIOMBEYA MUNGU


EWE WA FAKHARI – MWEMA WA MURUWA
ZIDI KUSUBIRI – KWANI WAELEWA
YAKUWA SAFARI – YATAKA KHATUWA

PILI NAKURAI – ATA SIKITIKO
ZIDI KUTUMAI – NAFUSINI MWAKO
KESHO KIWA HAI – NI MGENI MWAKO


NOMBEYA SALAMA – WANGU WA FUADI
NA WAKO MTIMA – NA UTABARADI
KIPENDA KARIMA – KUJA SINA BUDI

USIJIADHIBU – KWA KUWAZA SANA
SUBIRI MUHIBU – TUOMBE RABBANA
RAHA NA TAABU – TUTAPOKEZANA.

YOTE YANELEYA – SAMBI NI MZAHA
YANGAKULEMEYA – MAJONZI JARAHA
JUWA NAMI PIA – HUKU SINA RAHA

SI MIMI NI MOYO

SI MIMI NI MOYO - JAMANI WAPENDA
KWA MUNIONAYO- AMBAYO NATENDA


HEBU PULIKANI - MUFAHAMU KWANDA
LAWAMA NDA NINI - KWA NNAYO TENDA
SI MIMI JAMANI- NI MOYO WAPENDA


MUSINILAITI- JAMANI KWA HILI
NA MUKITAFITI- MUTAJUWA KWELI
APENDAE DHATI- LAWAMA HAJALI


BASI MUSEMAYO- ENYI MARAFIKI
NA MUNIONYAYO -SIKUWA SITAKI
NASHINDWA NA MOYO- HAUZUILIKIKWA KULA MUINDA -NI SILAHA NJEMA
NAMI TAJIPINDA -KUTORUDI NYUMA
MADAMU NAPENDA -SIJALI LAWAMA


KWELI NIWAMBIYE -MULOKUSANYIKA
NA MUSIDHANIYE -KUWA NITACHOKA
NI MIMI NI YEYE -KUZAMA KUZUKA


KUZAMA KUZUKA- KATU SIMUWATI
NA LITALOTUKA- KUBWA NI MUWATI
MNGU KIANDIKA- MJA HALIFUTI


HAPA TAKHATIMU -MBELE SITOKWENDA
KWAKE NI VIGUMU -MOYO KUUSHINDA
MUNGANILAUMU- NAYE ANIPENDA