OMBA NYIMBO

Add message
 • AHMEDFANI

  AHMEDFANI mombasa, coast province

  JUNGU LA FATANI " Jungu la Fatani Walilolipika Mungu melilani sasa mevundika Naanzaawali nduzapulikani Mwaloshitighali haki kufitini Nguvu za Jalali mewabwaga tini Jungu la Fatani Walilolipika Mungu melilani sasa mevundika Uzuzi na tani waloshikilia Waliwakizani wakapinga ndia Lakini Manani hakuwaridhia. Jungu la Fatani Walilolipika Mungu melilani sasa mevundika. Mwanzo wa kushika moto walowasha Ulibiririka uka ajaabisha sasa mezimika yao yamekwisha. Jungu la Fatani Walilolipika Mungu melilani sasa mevundika. Kusudio lao ni usizimike Lakini na wao sasa wakumbuke wakipanga yao Mngu ana yake. Jungu la Fatani Walilolipika Mungu melilani sasa mevundika. Mwanzo lengo lao walikifikiri kuwa moto wao utatukhasiri sasa nyuso zao zimetahayari. Jungu la Fatani Walilolipika Mungu melilani sasa mevundika. Moto kufuliza ni yao azima lakini muweza kwakuwa siwema aliunyunyiza maji ukazima. Jungu la Fatani Walilolipika Mungu melilani sasa mevundika. Tamati wendani mangi sitosema na lilo moyoni siidhini kupima Mujuwe Fatani hana mwisho mwema. Jungu la Fatani Walilolipika Mungu melilani sasa mevundika. .:love:

  JUNGU LA FATANI "

  Jungu la Fatani Walilolipika

  Mungu melilani sasa mevundika

  Naanzaawali nduzapulikani

  Mwaloshitighali haki kufitini

  Nguvu za Jalali mewabwaga tini

  Jungu la Fatani Walilolipika

  Mungu melilani sasa mevundika

  Uzuzi na tani waloshikilia

  Waliwakizani wakapinga ndia

  Lakini Manani hakuwaridhia.

  Jungu la Fatani Walilolipika

  Mungu melilani sasa mevundika.

  Mwanzo wa kushika moto walowasha

  Ulibiririka uka ajaabisha

  sasa mezimika yao yamekwisha.

  Jungu la Fatani Walilolipika

  Mungu melilani sasa mevundika.

  Kusudio lao ni usizimike

  Lakini na wao sasa wakumbuke

  wakipanga yao Mngu ana yake.

  Jungu la Fatani Walilolipika

  Mungu melilani sasa mevundika.

  Mwanzo lengo lao walikifikiri

  kuwa moto wao utatukhasiri

  sasa nyuso zao zimetahayari.

  Jungu la Fatani Walilolipika

  Mungu melilani sasa mevundika.

  Moto kufuliza ni yao azima

  lakini muweza kwakuwa siwema

  aliunyunyiza maji ukazima.

  Jungu la Fatani Walilolipika

  Mungu melilani sasa mevundika.

  Tamati wendani mangi sitosema

  na lilo moyoni siidhini kupima

  Mujuwe Fatani hana mwisho mwema.

  Jungu la Fatani Walilolipika

  Mungu melilani sasa mevundika.

  .love

 • Anubillu

  Anubillu Mombasa

  Dear Juma Bhalo, Naomba nyimbo ya EWE ULIYE JITUZA KWA SITAHA NA ADABU Thank you :love::love:

  Dear Juma Bhalo,
  Naomba nyimbo ya EWE ULIYE JITUZA KWA SITAHA NA ADABU

  Thank you
  lovelove

 • CuteIfaah

  CuteIfaah Dar

  Hey mamboz mm naomba kibao cha Kem kem

  Hey mamboz mm naomba kibao cha Kem kem

 • AHMEDFANI

  AHMEDFANI mombasa, coast province

  bwana admin mimi naomba unipe kibao cha "HARUFU YA NUNI' kibao hiki hunitoa roho, tuandikie shairi :bawling:

  bwana admin

  mimi naomba unipe kibao cha "HARUFU YA NUNI'
  kibao hiki hunitoa roho, tuandikie shairi bawling

 • mungah

  mungah USA

  HujamboBw Juma Bhalo. Nalikwenda katika website yako nyingine nikinuia kununua cds zako nilizozipenda miaka ya 70 na 80. Nikaacha ujumbe mwezi uliopita. Sijapata majibu tangu siku hio. Nilitaka kujua bei ( kwa shillingi)ya cds, dvds/vcds na cassettes. Ningependa kuzinunua nyimbo zote (pole pole)ulizoonyesha katika website yako.Sijui kama pia waweza pata za: Mwanahera. Maulidi Juma. Zuhura. Ali Mkali. Matano Juma. Rukia Ramadhani Malkia Rukia. Shakila na Sharmila. Omari Abu. Mamuni haji. Al-Watan Musical club. Yaani natafuta nyimbo za waimbaji wa miaka ya 60, 70, 80 na 90. Nijibu tafadhari.

  HujamboBw Juma Bhalo. Nalikwenda katika website yako nyingine nikinuia kununua cds zako nilizozipenda miaka ya 70 na 80. Nikaacha ujumbe mwezi uliopita. Sijapata majibu tangu siku hio. Nilitaka kujua bei ( kwa shillingi)ya cds, dvds/vcds na cassettes. Ningependa kuzinunua nyimbo zote (pole pole)ulizoonyesha katika website yako.Sijui kama pia waweza pata za:
  Mwanahera.
  Maulidi Juma.
  Zuhura.
  Ali Mkali.
  Matano Juma.
  Rukia Ramadhani
  Malkia Rukia.
  Shakila na Sharmila.
  Omari Abu.
  Mamuni haji.
  Al-Watan Musical club.
  Yaani natafuta nyimbo za waimbaji wa miaka ya 60, 70, 80 na 90.
  Nijibu tafadhari.

 • kidamani

  kidamani

  Salam Aleikum naomba shairi la KITINDWA Sina jaraha Nakipoa Sina kovu.:)

  Salam Aleikum naomba shairi la KITINDWA Sina jaraha Nakipoa Sina kovu.smile

 • don shushu

  don shushu tanga

  naomba mashairi ya sitara zambe kwa lopo

  naomba mashairi ya sitara zambe kwa lopo

 • MARYAM

  MARYAM MOMBASA

  NAOMBA SHAIRI LA SIKUDHANI KUWA TANIGEUKIYA NA MOYONI MWANGU SIKUFIKIRIYA MASIKINI KUMBE HANA MAZOWEYA:love::blush:

  NAOMBA SHAIRI LA SIKUDHANI KUWA TANIGEUKIYA NA MOYONI MWANGU SIKUFIKIRIYA MASIKINI KUMBE HANA MAZOWEYAloveblush

Maoni Ya Mashabik wa Juma Bhalo -

Board nameTopicsLast post

How to buy the songs

I need to buy mohamed juma bhalos old taarab music in dollars. Please list his music on ebay or amazon to make easy for me. Am a kenyan living in America. Reply soonest. This was sent via web form from your Bandzoogle site

106/15/2012 by Kijana Cha Juma Bhalo

wasifu wa mzee Bhalo by Remunga

Najisikia mwenye bahati kwa kupata jukwaa ambalo naweza kuyasoma, kununua, na hata kuzizikia sehemu tu ya nyimbo za mshairi niliyempenda, muimbaji aliyeikokota roho na kunituliza ukiwa tangu nilipokuwa kijana chipukizi aliyeyapenda mashairi yake kwa dhati. Nilipokuwa kijana wa miaka 14 hapo mwaka wa 1974, nilikuwa na madoea kuiyemelea redio ya baba(kumbuka nyakati hizo mzazi kuwa na redio...

0

General Board about Juma Bhalo

You can talk about anything here

306/13/2012 by ali